FALCAO atua Manchester United kwa mkopo wa mwaka mmoja

0 comments
MANCHESTER UNITED Imefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji Radamel Falcao kutoka Monaco baada ya mshambuliaji huyo kukubali kwenda Old Trafford kwa mkopo wa mwaka mmoja.

United Imefanikiwa kuzipiga bao Real Madrid, Manchester City na Arsenal ambazo zote kwa pamoja zilikuwa zinamuhitaji mshambuliaji huyo.


Falcao ataigharimu United pauni milioni 12 kwaajili ya dili hilo na sasa anaungana na Angel di Maria, Daley Blind, Luke Shaw, Ander Herrera na Marcos Rojo.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Colombia mwenye umri wa miaka 28, bado hajakubaliana maslahi binafsi na United lakini inaaminika amekwenda jijini Manchester kwa ndege ya kukodi kukamilisha kila kitu.

Soma Zaidi »

Loic Remy atua Chelsea

0 comments
CHELSEA imefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji “Loic Remy” wa QPR na kumsainisha mkataba wa miaka minne baada ya dau la pauni milioni 10.5 kukubaliwa.

Mchezaji huyo wa zamani wa Marseille ameiambia website ya Chelsea kuwa: “Nalijiskia furaha na fahari sana. Niliposikia Chelsea inanitaka nikasema ‘wache niende’ kwa sababu ni moja ya klabu bora duniani.


“Najiskia fahari na furaha kujiunga na Chelsea leo. Kwangu mimi ni jambo kubwa. Nina kiu kubwa ya kuungana na wachezaji wenzangu na kucheza mchezo wangu wa kwanza hapa.

“Nakumbuka msisimko wa kuvutia Stamford Bridge wakati nilipocheza mara ya kwanza pale nikiwa na Marseille na nashindwa kuvumilia kusubiri siku ya kucheza kwa mara ya kwanza mbele ya mashabiki wangu wapya.

“Niko hapa kwaajili ya kusaka maendeleo. Nina nafasi sasa ya kupata kilicho bora kupitia timu hii. Nahitaji kushinda mataji. Hii ndiyo sababu kwanini nimesaini Chelsea.”

Loic Remy alikuwa asainiwe na Liverpool wiki chache zilizopita lakini Liverpool wakamtosa dakika za mwisho kwa kusema mshambuliaji huyo amefeli vipimo vya afya.


Lakini kocha wa Chelsea Jose Mourinho amedai amehakikishiwa kuwa mshambuliaji huyo hana tatizo la kiafya litakaloathiri uchezaji wake.

Soma Zaidi »

SHINJI KAGAWA Atua rasmi Borussia Dortmund baada ya kukamilisha usajili wake

0 comments
HATIMAYE kiungo “Shinji Kagawa” amekamilisha usajili wake wa kujiunga na timu yake ya zamani Borussia Dortmund kwa dau la pauni milioni 12.5 akitokea Manchester United.

Borussia Dortmund imetangaza rasmi kupitia Website ya Klabu hiyo kuwa kiungo huyo wa kimataifa wa Japan amejiunga nao tena baada ya kukaa Old Trafford kwa misimu miwili.


Kagawa mwenye miaka 27, ameichezea United mara 57 na kufunga magoli 6 ikiwemo hat-trick dhidi ya Norwich City.

“Nilisema tangu mwanzo wakati naondoka hapa kuwa historia yangu na Borussia Dortmund bado haijakamilika,” Kagawa aliuambia mtandao wa Borussia Dortmund na kuongeza: “Dortmund ni kama familia na nashukuru kuwa hawajanisahau.”

Soma Zaidi »

CHELSEA yazidi kutesa Ligi kuu England….yaitandika EVERTON 6-3

0 comments
CHELSEA imezidi kujiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya kuitandika Everton 6-3 ugenini.

Mshambuliaji mpya wa Chelsea Diego Costa Ndiye aliyekuwa wa kwanza kuipatia Chelsea goli la kuongoza katika dakika 1 kipindi cha kwanza na kuhitimisha karamu hiyo ya magoli kwa kufunga tena goli katika dk 90 kipindi cha pili.


Magoli mengine ya Chelsea yalifungwa na Branislav Ivanovic dakika ya 3, goli la kujifunga la Seamus Coleman dakika ya 67 na Nemanja Matic dakika ya 74 na Ramires dakika ya 77.

Magoli ya Everton yalifungwa na Kevin Mirallas dakika ya 45, Steven Naismith dakika ya 69 na Samuel Eto’o dakika ya 76.

Katika mchezo huyo kikosi cha Chelsea kiliwakilishwa na: Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Matic,Willian (Mikel 75),Fabregas (Drogba 89),Hazard (Luis 83), Costa.

Wakati kikosi cha Everton kiliwakilishwa na: Howard, Coleman, Jagielka, Distin, Baines, McCarthy, Barry, Mirallas, Naismith, McGeady (Eto'o 70), Lukaku (Besic 89).

Soma Zaidi »

MANCHESTER UNITED yakubali kumsajili “DALEY BLIND” kwa dau la pauni milioni 13.8

0 comments
MANCHESTER United Imekubali kutoa dau la pauni milioni 13.8 kwaajili ya kumsajili beki kisiki “Daley Blind” kutoka Ajax  ya Uholanzi.

Manchester United na Ajax wamekubaliana dau hilo siku ya Ijumaa, na mchezaji huyo anatarajia kufanya mazungumzo na Manchester United kuhusu masuala binafsi, ambayo ni lazima atimize.


Beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi hakuwepo katika kikosi cha Ajax kilicho cheza mechi dhidi ya Groningen siku ya Jumapili baada ya kupewa ruhusa kwenda kufanya mazungumzo na United.

Blind mwenye umri wa miaka 24 ana uwezo wa kucheza kama beki wa kushoto, beki wa kati na kiungo mkabaji na anatarajia kufanya vipimo vya afya siku ya Jumapili jijini Manchester kabla ya kujiunga na united.

Kupitia akaunti yao ya Twitter United wamesema kuwa: ‘Manchester United imekubaliana na Ajax kumsajili beki Daley Blind, kinacho fuatia ni vipimo vya afya na masuala binafsi.Matangazo mengine yatafuta kila kitu kitakapo kamilika.’

Blind anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na united msimu huu baada ya kusajiliwa kwa Angel di Maria, Marcos Rojo, Ander Herrera na Luka Shaw.

Soma Zaidi »

SHINJI KAGAWA Arudi Borussia Dortmund Kwa pauni milioni 8

0 comments
HATIMAYE kiungo wa Manchester United Shinji Kagawa ametimka Old Traford na Kurudi katika klabu yake ya zamani Borussia Dortmund.

Kocha wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp ameweka wazi kuwa Kagawa anakaribishwa milango iko wazi, bosi huyo anamatumaini ya kumpata mchezaji huyo kutokana na Kagawa kushindwa kupata namba ya kudumu,anarejea Borussia Dortmund kwa dau la pauni milioni 8.


Kagawa alijiunga na Manchester United Julai 2012 akitokea Dortmund kwa dau lenye thamani ya pauni milioni 12, Lakini amekuwa akikabiliwa na Majeruhi ya mara kwa mara.

Nyota huyo wa kimataifa wa Japani anatarajiwa kuwasili Ujerumani siku ya Ijumaa kwaajili ya kukamilisha usajili huo ambao utakuwa wa miaka minne.

Soma Zaidi »

Ajali yaua watu kumi na kujeruhi saba mbeya

0 comments
 WATU kumi wakiwemo watoto wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine saba wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari mawili.

Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa nne asubuhi ikihusisha gari ndogo ya abiria maarufu daladala lenye namba za usajili T 237 BFB aina Toyota Hiace  na gari kubwa aina ya Fuso lenye namba za usajili T 158 CSV.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo ilitokea maeneo ya Mbalizi baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea Mbeya mjini kuelekea Mbalizi kulivaa Fuso lililokuwa likiingia barabarani.

Walisema inasemekana dereva wa Hiace gari yake ilimshinda kutokana na kutelemka mlima mkali wa Mbalizi inagawa pia walimtupia lawama dereva wa Fuso ambaye alikuwa akiingia barabarani bila kuchukua tahadhari.

Muuguzi Mkuu wa Hospitali teule ya Ifisi Mbalizi, Sikitu Mbilinyi, ambako Majeruhi na marehemu walikimbizwa hapo alithibitisha kupokea majeruhi 7 ambapo alisema kati yao ni wanawake 3 na wanaume 4.

Alisema kati ya majeruhi hao wawili wamepewa rufaa kwenda hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na kuhitaji msaada zaidi huklu wengine wakiendelea kupatiwa msaada wa haraka ili kunusuru hali zao.

Mbilinyi aliongeza kuwa pia wamepokea miili ya marehemu 10 wakiwemo watoto wawili na Wanawake wanne na Wanaume wanne.

Hata hivyo majina ya majeruhi na marehemu hayajaweza kupatikana mara moja kutokana na kuwa katika hali mbaya ambapo Dereva wa Fuso akitokomea mara baada ya tukio hilo.

Soma Zaidi »

Xabi Alonso ajiunga na Bayern Munich

0 comments
BAYERN MUNICH wamethibitisha kumsajili kiungo Xabi Alonso kutoka Real Madrid kwa dau lenye thamani ya wastani wa euro milioni 10.

Kiungo huyo mwenye miaka 32 amesani mkataba utakao mwezesha kukaa Allianz Arena mpaka mwaka 2016 chini ya kocha wa zamani wa Barcelona Pep Guardiola.

Alonso,ambaye ametangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Hispania siku ya jumatano,baada ya timu hiyo kutolewa mapema katika hatua ya makundi katika michuano ya kombe la dunia iliyo fanyika nchini Brazil mwaka huu,amekuwa na mabingwa wa Ulaya tangu alipojiunga kwa ada iliyofanywa siri akitokea Liverpool miaka mitano iliyopita.

Kusajiliwa kwa Toni Kroos kutoka Bayern na James Rodriguez kutoka Monaco kama viungo, kumesababisha Alonso aombe kuondoka mapema katika dirisha hili la usajili baada ya kupoteza namba katika kikosi hicho.

Alonso anatarajiwa kuongeza nguvu katika nafasi ya kiungo wa kati wa Bavarians, kufuatia kutokuwepo kwa viungo Javi Martinez, Bastian Schweinsteiger na Thiago Alcantara ambao wameumia.

Kiungo wa zamani wa Bayern Luiz Gustavo, anajiandaa kuondoka Wolfsburg kwenda Santiago Bernabeu kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Alonso.

Soma Zaidi »

Akutwa amejinyonga shambani na kuacha ujumbe,“Nawaachia dunia yenu muishi miaka 110”

0 comments
Mtu mmoja ambaye hakujulikana jina, amekutwa akiwa amejinyonga ndani ya kibanda shambani huku akiwa na karatasi iliyoandikwa ujumbe “Nawaachia dunia yenu muishi miaka 110”.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kibiki, Ally Hussein alisema kijana huyo mwanamume amekutwa saa mbili usiku akiwa amefariki na hivyo kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Chalinze.

Alisema askari walifika na kuukuta mwili wa marehemu ukiwa umefungwa kamba ya katani na alipopekuliwa alikutwa mfukoni na karatasi yenye maandishi hayo.


Kaimu Kamanda wa Polisi Pwani, Mrakibu msaidizi, Athumani Mwambalaswa amethibitisha tukio hilo na kusema mwili wa marehemu ulichukuliwa na kuifadhiwa Kituo cha Afya Chalinze kusubiri uchunguzi wa daktari.

Hata hivyo, alisema bado haijafahamika mtu huyo ni mwenyeji wa kijiji kipi kwani hapo Kibiki hakuweza kutambulika na jitihada za kutafuta ndugu zake katika vijiji vya jirani zinafanyika. Chanzo cha kujinyonga bado hakijajulikana.

Soma Zaidi »

Ronaldo amtaka Di Maria kuitendea haki jezi namba saba Man Utd

0 comments
MCHEZAJI BORA wa UEFA barani Ulaya Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro amemtakia kila la kheri mshambuliaji mpya wa Manchester United Ángel Fabián Di María Hernández katika majukumu yake akiwa Old Trafford.

Ronaldo ambaye alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa uefa barani Ulaya jana jioni kwa kuwashinda wapinzani wake Manuel Neuer pamoja na Arjen Robben amesema anatambua uwezo wa Di Maria uwanjani na unaweza kufanya mageuzi makubwa katika kikosi cha Manchester United.

Lakini pamoja na kumtumia salamu za kumtakia kheri Ronaldo amemtaka Di Maria kuitendea haki jezi namba saba aliyokabidhiwa kwa kumueleza kwamba jezi hiyo ina majukumu makubwa.


Amesema wakati akisajiliwa na  Manchester United mwaka 2003 alikabidhiwa jezi namba saba ambayo ulikuwa inatumiwa na gwiji wa soka nchini Uingereza David Robert Joseph Beckham na bila ajizi aliitendea haki jezi hiyo kwa kufanya kusudio la kuibeba Manchester United wakati wote.

Hata hivyo Di Maria amekiri ni kweli alielezwa maneno hayo na Ronaldo na ameahidi kufanya kila jitihada ili kutimiza kusudio la kurejesha fadhila Manchester United. Di Maria alitambulishwa rasmi kwa waandishi wa habari hapo jana.

Soma Zaidi »

Juventus wakataa ofa ya Manchester United

0 comments
MABINGWA wa soka nchini Italia Juventus wametunisha msuli kwa kuikataa ofa ya Manchester United  ambayo ilikuwa na lengo la kumsajili kiungo mshambuliaji kutoka nchini Chile Arturo Vidal.

Kwa mujibu wa gazeti la michezo la nchini Italia Gazzetta Dell Sport Juventus wamekataa ofa ya Euro million 43, ambayo iliwekwa mezani na Manchester United  kwa imani kwamba ingetosha kuwashawishi juventus kufungua mazungumzo ya kumsajili Vidal.


Kukataliwa kwa ofa hiyo kunaelezwa kama sababu nyingine kwa Juventus kuonyesha dalili za kuendelea kubaki na mchezaji huyo, ama kumuuza kwa ada kubwa ya usajili ambayo huenda wakaitumia kwa kufanya usajili wa wachezaji zaidi ya wawili.

Lakini kwa upande wa Manchester United  ambao wanapewa ushawishi mkubwa na meneja Louis van Gaal, haujazungumza lolote juu ya suala la kuwasilishwa kwa ofa hiyo huko mjini Turin.

Soma Zaidi »

Xabi Alonso anakaribia kutua Bayern Munich baada ya kufaulu vipimo vya afya Ujerumani

0 comments
XABI ALONSO anajiandaa kukamilisha usajili wake wa pauni milioni 7.5 kutoka Real Madrid kwenda Bayern Munich siku ya Ijumaa.

Alonso mwenye miaka 32 aliwasili Munich, Ujerumani siku ya Alhamisi kwaajili ya vipimo vya afya akiwa na daktari wa timu hiyo Bw.Hans-Wilhelm Mueller-Wohlfahrt.

Kiungo huyo wa zamani wa Liverpool alikuwa akihusishwa na tetesi za kujiunga na Manchester United baada ya kukaa Bernabeu kwa muda wa miaka mitano, lakini amechagua kujiunga na Pep Guardiola.

Mpango wa Alonso kujiunga na mabingwa hao wa Ujerumani umekuja baada ya kuumia kwa viungo Thiago Alcantara, Bastian Schweinsteiger na Javi Martinez.

Mkurugenzi wa Michezo Matthias Sammer anaamini Alonso ataipa Bayern changamoto mpya, alisema: “Kama tutafanikiwa, nitakuwa na hisia nzuri sana kwa kocha na klabu.

“Baada ya kuumia kwa Thiago na Schweinsteiger tumekuwa tukiangalia mtu, ambae anaweza kutusaidia mara moja. Na Xabi Alonso anaweza kucheza katika kiwango cha juu kwa miaka miwili.”

Nae mwenyekiti wa Bayern Jan-Christian Dressen amesema kuwa wako katika hatua za mwisho kumilisha dili hilo na Real.

“Tumesha kubaliana na Xabi Alonso. Na nina matumaini tutahafikiana na Real Madrid katika siku moja au mbili zijazo,” alisema.

‘Hatuzungumzii kuhusu mkopo,huu utakuwa usajili wa kudumu.’

Soma Zaidi »
Copyright © 2013. Bloggermdodosaji.com - All Rights Reserved
Customized by: MdodosajiBlog Tz | Powered by: Mdodosaji
Designed by: Mdodosaji